MAN CITY YAKATAA OMBI LA WAJERUMANI BAADA YA KUAHIRISHWA MECHI JANA, BARCELONA YAMTWISHA BR MZIGO WA MAGOLI
Pambano la ligi ya mabingwa barani Ulaya kati ya wenyeji Manchester City na Wajerumani Borussia Monchengladbach liliahirishwa jana baada ya mvua kubwa iliyoambatana na radi kutishia usalama wa mchezo huo.
Kufuatia kuahirishwa pambano hilo la kundi C kikao cha upangaji muda wa kufanyika pambano hilo kilipanga leo ichezwe mechi hiyo japokua ombi lilipopelekwa na Wajerumani lilikataliwa.
Sheria za Uefa zinataka pambano linaloahirishwa kuchezwa siku inayofata na ndicho kilichofanyika lakini Wajerumani walitaka pambano hilo kuanza saa 12 jioni kwa saa za UK badala ya saa 1 na dakika 45 ya muda wa kawaida ili waweze kusafiri kurudi Ujerumani baada ya mechi.
Ombi hilo lilikataliwa na wenyeji Man City na kuahidi kutoa vyumba 38 katika hostel ya klabu hiyo kwaajili ya wageni hao ombi ambalo Borussia hawakuridhika nalo.
Katika mechi nyingine ya kundi hilo Wenyeji Barcelona waliifunga Celtic ya Scotland inayofundishwa na kocha wa zamani wa Liverpool Brendan Rodgers (BR) bao 7-0.
Lionel Messi alifunga bao hat-trick, Suarez akafunga bao 2 huku Andreas Iniesta na Neymar wakifunga bao moja moja.

No comments