SIMBA HATI HATI KUMKOSA IBRAHIM AJIBU MECHI DHIDI YA YANGA

Vinara wa ligi kuu Tanzania bara Simba inaweza kumkosa mshambuliaji wake tegemezi Ibrahim Ajibu Migomba watakapoivaa Yanga Oktoba Mosi.


Tayari Ibrahim Ajibu ambaye huwasumbua vilivyo mabeki wa timu pinzani ana kadi mbili za njano na kama Simba watamtumia katika mechi ya Jumamosi dhidi ya Majimaji ya Songea na akapata kadi ya tatu ya njano basi atatakiwa kuukosa mchezo unaofata ambao utakua dhidi ya Yanga.

Ni wajibu wa Kocha Joseph Omog kumpumzisha Ajibu siku ya Jumamosi ili kumlinda asipate kadi ya njano au kumchezesha na Ajibu mwenyewe ajichunge asipate kadi yoyote siku hiyo.

Bado Simba ina wachezaji wengi wanaoweza kucheza nafasi ya Ajibu kama atakosekana katika mchezo dhidi ya Majimaji mmoja wapo akiwa ni Mu Ivory Coast Fredrick Blagnon au Haji Ugando.

No comments

Powered by Blogger.