SERENGETI BOYS WAELEKEA NJE YA NCHI KUJIANDAA DHIDI YA CONGO

Kikosi cha nyota 21 wa timu ya Taifa ya Tanzania ya vijana wenye umri wa chini ya miaka 17 ‘Serengeti Boys’, kimeondoka jana alfajiri Septemba 4, 2016 kwa kwenda jijini Victoria, kwenye Kisiwa cha Mahe nchini Shelisheli kwa ajili ya kupiga kambi kujiandaa na mchezo dhidi ya Congo-Brazzaville utakaofanyika Septemba 18, mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Serengeti Boys itacheza na Congo-Brazzaville katika mchezo wa kwanza jijini Dar es Salaam kuwania nafasi ya kucheza fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa vijana wenye umri wa chini ya miaka 17. Fainali za vijana zitafanyika mwakani nchini Madagascar.
Itakumbukwa kwamba Benchi la ufundi lilimshauri Rais wa TFF, Jamal Malinzi kwamba kambi hiyo ipigwe Shelisheli. Hii ni mara ya pili kwa Malinzi kutimiza ahadi yake kwa wachezaji hao. Kwa mara ya kwanza aliahidi kuwapa kambi ya nje kama wangewatoa Shelisheli.
Timu kweli ilikwenda Madagascar kabla ya kuivaa Afrika Kusini ‘Amajimbos’ na kuitoa na kwa sasa inakwenda Shelisheli kujipanga kwa ajili ya kuitoa Congo-Brazzaville katika harakati za kuwania nafasi ya kucheza Kombe la Mataifa ya Afrika kwa vijana.

No comments

Powered by Blogger.