LICHA YA KUPATA USHINDI MFULULIZO SIMBA "WAUKATAA" UWANJA WA UHURU
Vinara wa ligi kuu Tanzania Bara Simba SC wametuma barua kwa bodi ya ligi wakitaka kusitisha mechi zao kupigwa katika dimba la Uhuru jijini.
Katika barua yao iliyosainiwa na katibu mkuu wake Patrick Kahemele ambayo www.wapendasoka.com imepata nakala yake, Simba wamelalamikia usalama wa wachezaji wao na Malalamiko ya mashabiki wao kushindwa kuingia uwanjani katika mechi dhidi ya Azam FC.
Katika lalamiko lao la msingi Simba wanalalamikia kukauka kwa plastiki zinazoshika nyasi bandia hali iliyopelekea wachezaji kuchubuka na kupata majeruhi.
Pia kitendo cha Mashabiki wengi kushindwa kuingia uwanjani Jumamosi wakati timu hiyo ilipokua ikimenyana na Azam FC kimelalamikiwa na klabu hiyo ikiwa ni kitendo kilichowakosesha mashabiki wake burudani pamoja na kuikosesha klabu mapato.
Ombi lao la msingi baada ya malalamiko hayo ni kuomba kuendelea kutumia uwanja wa Taifa kama ilivyokua awali.
Unaweza kuisoma kwa kirefu barua hiyo ya Simba hapa

No comments