KIKOSI CHA TAIFA STARS WATAKAOIVAA ETHIOPIA HIKI HAPA.

Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Charles Boniface Mkwasa ametaja majina ya nyota 24 watakaounda kikosi ambacho kitasafiri mwishoni mwa wiki ijayo kwenda Addis Ababa, Ethiopia kucheza na wenyeji wetu kwenye mchezo wa kirafiki wa kimataifa utakaofanyika Oktoba 8, mwaka huu.



Mkwasa amesema wachezaji aliowaita wataingia kambini Oktoba 2, 2016 kabla ya kuanza kukiandaa kuanzia Oktoba 3, 2016 ikiwa mara baada ya michezo ya Ligi Kuu Tanzania Bara ya mwishoni mwa wiki hii.

Makipa

Deogratius Munishi – Young Africans
Said Kipao – JKT Ruvu
Aishi Manula – Azam FC

Mabeki

Shomari Kapombe – Azam FC
Juma Abdul – Young Africans
Vicent Andrew - Young Africans
Mwinyi Haji - Young Africans
Mohamed Hussein – Simba SC
David Mwantika - Azam FC
James Josephat – Tanzania Prisons

Viungo wa Kati

Himid Mao - Azam FC
Mohammed Ibrahim – Simba SC
Jonas Mkude – Simba SC
Muzamiru Yassin – Simba SC
Viungo wa Pembeni

Shiza Kichuya – Simba SC
Simon Msuva - Young Africans
Juma Mahadhi - Young Africans
Jamal Mnyate – Simba
Hassan Kabunda – Mwadui FC

Washambuliaji

Ibrahim Ajib – Simba SC
John Bocco - Azam FC
Mbwana Samatta - CK Genk ya Ubelgiji
Elius Maguli – Oman
Thomas Ulimwengu – TP Mazembe Congo

 Mchezo huo utakaofanyika jijini Addis Ababa, umeratibiwa kwa mujibu wa kalenda ya Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) ambalo huwa na kalenda ya wiki ya mechi za kimataifa kwa wanachama wake ambao Tanzania ni miongoni mwao.

No comments

Powered by Blogger.