HIZI NDIZO MECHI AMBAZO KEVIN DE BRYUNE ATAZIKOSA BAADA YA KUUMIA
Moja ya nguzo muhimu katika kikosi cha Manchester City msimu huu ni kiungo Kevin De Bryune ambaye taarifa zimetoka kwamba atakua nje kwa muda wa mwezi mmoja.
De Bryune Raia wa Ubelgiji alipata majeraha ya misuli ya paja Wikiend iliyopita wakati Man City walipoifunga Swansea bao 3-1.
Kufuatia hali hiyo imefahamika kwamba De Bryune atakosa mechi ya kesho Ligi ya mabingwa Ulaya dhidi ya Celtic, Tottenham Hotspur wikiend hii,Atashindwa kuiwakilisha nchi yake katika pambano lao dhidi ya Bosnia na Gibratar na ile mechi ya ligi kuu dhidi ya Everton.
Japokua madaktari wanafanya kila liwezekanalo mchezaji huyo apone mapema kabla ya mechi dhidi ya Barcelona katikati ya mwezi ujao.
Hilo ndio jembe kwa sasa, daahh, inatugharimu sana
ReplyDelete