HII HAPA RATIBA YA LIGI YA MABINGWA ULAYA LEO : DORTMUND KUWAKARIBISHA MABINGWA REAL MADRID,LEICESTER NA FC PORTO

Hatua ya pili ya mechi za makundi katika michuano ya Ligi ya mabingwa barani Ulaya inapigwa leo naakesho barani humo.



Mabingwa watetezi Real Madrid baada ya kulazimishwa sare katika mechi mechi ya ligi kuu ya Spain dhidi ya Las Palmas leo itasafiri kuwavaa wakali toka Bundesliga Klabu ya Borussia Dortmund.

Dortmund iliyo katika kiwango bora ikishinda kwa bao 3-1 katika mechi yake ya Bundesliga dhidi ya Freiburg itaingia katika dimba la Signal Induna park ikiwa na safu bora kabisa ya ushambuliaji.

Mechi zingine leo mabingwa wa England Leicester City watawàalika mabingwa wa Ureno FC Porto mechi insyotarajiwa kuchezwa katika dimba la King Power ikiwa ni mara ya kwanza kwa dimba hilo kuchezwa ligi ya mabingwa.

Tottenham baada ya kufungwa katika mechi ya awali dhidi ya Monaco itasafiri kuikabili CSKA Moscow toka Russia.

Mechi zote hizi zitaanza majira ya saa 4 kasoro usiku kwa saa za hapa nyumbani.


No comments

Powered by Blogger.