DTB YAMWAGA MAMILIONI KUIDHAMINI LIGI KUU TANZANIA BARA

Benki ya Dimond Trust yenye makao yake makuu jijini Dar es Salaam imeingia makubaliano na shirikisho la Soka Tanzania TFF kuidhamini Ligi kuu ya Vodacom

DTB inaongeza idadi ya wadhamini wa ligi hiyo inayoshika kasi hivi sasa kwa kusaini mkataba wa fedha za Kitanzania milioni 250 kwa mwaka pesa ambazo zitaongeza chachu ya ligi hiyo.

Mkataba huo umesainiwa jijini Dar Es Salaam na mkuu wa Kitengo cha fedha cha Benki hiyo Joseph Mabusi na Rais Wa TFF Jamal Malinzi katika hoteli ya Serena.

Mgawanyo wa fedha hizo haujawekwa Wazi lakini ni dhahiri utaongeza kiwango cha pesa kwa vilabu shiriki hali ambayo itaongeza ushindani.

No comments

Powered by Blogger.