CRYSTAL PALACE YAMSAJILI KIUNGO MKONGWE WA ARSENAL

Klabu ya Crystal Palace imekamilisha usajili wa kiungo Methieu Flamini kama mchezaji huru kwa mkataba wa mwaka mmoja.

Flamini mwenye miaka 32 aliyeachwa na Arsenal baada ya kumalizika kwa msimu uliopita alikua mchezaji huru ambaye angeweza kusajiliwa na klabu yoyote licha ya dirisha la usajili kuwa tayari limeshafungwa.

Flamini raia wa Ufaransa aliichezea Arsenal michezo 246 kwa vipindi viwili tofauti akishinda kombe la FA mara 3 na kufunga mara 12.

Amewahi kuichezea pia AC Milan kwa miaka mitano na kushinda ubingwa wa Italia Serie A mara moja yani mwaka 2011 anakua mchezaji wa Tano kusajiliwa na kocha Alan pawdew wa Crystal Palace wengine ni Andros Townsend, Steve Mandanda, James Tomkins na Christian Benteke huku loic remy akijiunga na klabu hiyo kwa mkopo wa msimu mzima toka Chelsea.


No comments

Powered by Blogger.