YANGA YAZIKATAA JEZI ZILIZOTOLEWA NA MDHAMINI WA LIGI KUU

Mabingwa wa kandanda wa Tanzania bara Yanga wamezikataa jezi zilizotolewa na mdhamini wa ligi kuu Tanzania bara kampuni ya Vodacom.



Akiongea Dar es Salaam leo mjumbe wa kamati ya Utendaji ya Yanga na meneja wa masoko Omary Kahaya ametoa sababu mbalimbali za kuzikataa jezi hizo.

Kahaya amezitaja sababu hizo kuwa ni

1. Hawakushirikishwa katika utengenezaji na ubunifu wa jezi hizo.

2. Ubora wake ni wa hali ya chini.

3. Jezi ya ugenini inafanana na ya msimu uliopita hivyo itakua ngumu kufanya biashara ya jezi hizo.

No comments

Powered by Blogger.