RONALDO NDANI, MESSI NJE TUZO YA MCHEZAJI BORA ULAYA

Majina ya wachezaji watatu yamebaki katika orodha ya wachezaji wanaowania tuzo ya mchezaji bora wa Ulaya kwa msimu wa mwaka 2015/2016 ambao ni Cristiano Ronaldo,Gareth Bale wa Real Madrid na Antonio Griezman wa Atletico Madrid.



Mshindi wa tuzo hizo atatangazwa Agosti 25 mwaka huu wakati wa Upangaji wa makundi ya Ligi ya Mabingwa barani Ulaya kwa kupigiwa kura.

Cristiano Ronaldo ndiye anayeshikiria tuzo hiyo baada ya kuitwaa mwaka jana akiwania nafasi ya kishinda tuzo hiyo kwa mara ya pili.


No comments

Powered by Blogger.