VIJANA WATANO TOKA KIGAMBONI NA TEMEKE WAULA AZAM FC, JUMAMOSI HII NI ZAMU YA ILALA
Mpango wa kukuza Vipaji vya soka unaoendeshwa na mabingwa wa Afrika Mashariki na kati Azam FC ulianza tena juzi Jumamosi kwa program maalumu iliyofanyika katika dimba la Azam Complex Chamazi Jijini Dar es Salaam.
Azam chini ya Mkuu wa Soka la Vijana Tom Legg waliendesha kliniki maalumu iliyohusisha vijana wenye umri wa miaka chini ya 17 katika wilaya za Kigamboni na Temeke.
Jumla ya vijana 424 walijitokeza katika kliniki ya soka la vijana hiyo Jana Jumapili na kati ya hao vijana watano tu ndiyo waliofanikiwa kupata nafasi ambao watajiunga na timu ya vijana ya Azam.
Azam FC itaendelea na kliniki hiyo nchi nzima ili kuweza kupata vijana sahihi kwa klabu hiyo na kwa Taifa na wiki hii kliniki hiyo kwa vijana wa Ilala.
Kwa kijana yeyote mwenye kipaji anatakiwa kufika katika viwanja vya Jakaya Kikwete (Zamani kidongo Chekundu) kaunzia saa 1 kamili Asubuhi.
![]() |

No comments