MECHI YA YANGA NA JKT RUVU YAPIGWA KALENDA

Mechi ya kiporo ya ligi kuu Tanzania Bara kati ya Yanga na JKT Ruvu iliyopangwa kufanyika Jumatano hii imeahirishwa.



Bodi ya Ligi Kuu nchini Tanzania (TPLB) ambayo iko chini ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), imethibitisha kuwa mchezo huo uliopangwa kufanyika katika Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam umeahirishwa mpaka itakapopangiwa tarehe nyingine.

Mechi hiyo imeondolewa kutokana na timu ya Yanga kuwa na wachezaji wengi kwenye kikosi cha timu ya Taifa (Taifa Stars) kinachosafiri Agosti 31, 2016 asubuhi kwenda Lagos, Nigeria kwa ajili ya mechi ya mchujo ya michuano ya Kombe la Afrika (AFCON Qualifiers) itakayochezwa Septemba 3, 2016.
Mabadiliko hayo hayatavuruga ratiba ya mechi zinazofuata za Ligi Kuu ya Vodacom kwa timu husika.

Tayari wahusika wakiwamo Yanga na JKT Ruvu SC, wamejulishwa.

No comments

Powered by Blogger.