UEFA SUPER CUP: SEVILLA YASHINDWA KUCHUKUA UBINGWA KWA MARA YA 3 MFULULIZO,REAL MADRID WATWAA TENA

Pazia la ligi ya mabingwa na michuano ya Europa League barani Ulaya lilifunguliwa jana kwa mechi ya Super Cup kati ya Real Madrid na Sevilla zote za Spain.

Mechi hiyo ilimalizika kwa ushindi wa bao 3-2 Real Madrid ambao ni mabingwa wa Ligi ya mabingwa Ulaya na Sevilla ambao ni mabingwa wa Europa League.

Real Madrid walitangulia kupata bao likifungwa na kiungo chipukizi Marco Willemsen huku Sevilla wakisawazisha kwa bao la kiungo Franco Vazquez na kufanya mchezo huo kwenda mapumziko magoli yakiwa 1-1.

Kipindi cha pili Sevilla walipata penati iliyofungwa na Yehven Konoplyanka kabla ya nahodha Sergio Ramos hajasawazisha muda wa nyongeza na kufanya mchezo huo kumalizika kwa sare ya bao 2-2 ndipo zikaongezwa dakika 30 na Real Madrid wakapata bao la ushindi kupitia kwa beki wa pembeni Dani Calvajal.

No comments

Powered by Blogger.