FRANK DE BOER ATANGAZA MIPANGO MIWILI YA KUANZIA INTER MILAN

Kocha mpya wa Inter Milan Mholanzi Frank De Boer ameweka wazi mipango yake miwili ambayo anataka kuifanya katika klabu hiyo.

De Boer amenukuliwa na gazeti maarufu la michezo nchini Italia "Gazzetta dello Sport"  toleo la leo akisema kwamba mipango hiyo miwili ndiyo atakayoanza nayo katika ujenzi mpya wa Inter Milan.

Mpango wa kwanza ni kuhakikisha mshambuliaji anayewaniwa na vilabu vingi kwasasa barani Ulaya Mauro Icardi haondoki klabuni hapo lakini mpango wa pili ni kuipa changamoto Juventus katika ubingwa wa Serie A.

No comments

Powered by Blogger.