TING YAZINDUA CHANELI MPYA ZA MICHEZO, NI YA KWANZA TANZANIA
Kituo cha Luninga cha Tanzania Intergrated Network Group (TING) kinachorusha matangazo yake toka Mbezi Jijini Dar es Salaam leo kimefanya mapinduzi makubwa katika tasnia ya michezo.
TING Imezindua Chaneli mbili mahususi za michezo kupitia king'amuzi chao, Chaneli ambazo ni mahususi kwaajili ya kukuza na kuendeleza michezo nchini.
Akizindua Channel hizo mbili zitakazojulikana kama TING HD MICHEZO 1 na TING HD MICHEZO 2 naibu waziri wa Habari Sanaa,Utamaduni,Wasanii na Michezo Anastazia James Wambura amemshukuru Mmiliki wa kituo hicho na kumpongeza kwa juhudi kubwa anazozionyesha katika kuinua michezo nchini.
Waziri Wambura pia alisisitiza dhana kubwa ya Serikali ya kutaka kuwekeza katika viwanda,ajira na michezo na akawaomba wadau wengine kujitokeza kuunga mkono jitihada za serikali ili watanzania wengi wanufaike na michezo.
Awali akitoa neno kuhusu kuanzishwa kwa chaneli hizo mbili Mkurugenzi mkuu wa kituo hicho Dr. Vernow Fernandos alisema " Baada ya kuwekeza kwa kiwango kikubwa katika kuonyesha michezo mbalimbali ya nje ya nchi ikiwemo mechi za ligi kuu ya England na michuano ya ligi ya mabingwa Ulaya,walifikiria kuja na kitu tofauti kitakachoinufaisha michezo yetu hapa Tanzania na kuitangaza zaidi"
Dr. Fernandos aliendelea kueleza kwamba "Mpango huu wa kuwekeza katika michezo utakuza michezo yetu na kututangaza zaidi pamoja na kutoa ajira kwa vijana wetu na tayari ajira zaidi ya 80 zimeshatolewa na kituo hicho".
Chaneli hizo mbili za michezo zitakua na vipindi mbalimbali ambavyo Meneja Mkuu wa vipindi katika kituo hicho Bwana Dennis Msemwa alivitaja kuwa ni pamoja na:-
● Kandanda Kijiweni - Hii itajikita kupata maoni ya mashabiki makocha na wadau wa Soka.
● Sports News - Hii itahusisha taarifa mbalimbali za michezo ndani na nje
● Kandanda Show - Hii itahusisha uchambuzi wa mechi mbalimbali za soka duniani.
● The Profile - Hii itahusisha habari za wanamichezo mbalimbali,Historia na maisha yao.
● Asili yetu - Hii itahusisha utambulishwaji wa Utamaduni wa Mtanzania hasa upande wa Sanaa na wasanii.
● Art and Talent - Hii itahusisha kuvumbua vipaji na kuonyesha vipaji mbalimbali katika jamii.
Kituo hicho kinakua cha kwanza nchini Tanzania kuzindua Chaneli zenye lengo la kukuza na kuendeleza michezo hapa nchini.
![]() |
Naibu Waziri Wambura akikata utepe kuzindua chaneli mpya |
Akizindua Channel hizo mbili zitakazojulikana kama TING HD MICHEZO 1 na TING HD MICHEZO 2 naibu waziri wa Habari Sanaa,Utamaduni,Wasanii na Michezo Anastazia James Wambura amemshukuru Mmiliki wa kituo hicho na kumpongeza kwa juhudi kubwa anazozionyesha katika kuinua michezo nchini.
![]() |
Dr. Fernandos |
Awali akitoa neno kuhusu kuanzishwa kwa chaneli hizo mbili Mkurugenzi mkuu wa kituo hicho Dr. Vernow Fernandos alisema " Baada ya kuwekeza kwa kiwango kikubwa katika kuonyesha michezo mbalimbali ya nje ya nchi ikiwemo mechi za ligi kuu ya England na michuano ya ligi ya mabingwa Ulaya,walifikiria kuja na kitu tofauti kitakachoinufaisha michezo yetu hapa Tanzania na kuitangaza zaidi"
Dr. Fernandos aliendelea kueleza kwamba "Mpango huu wa kuwekeza katika michezo utakuza michezo yetu na kututangaza zaidi pamoja na kutoa ajira kwa vijana wetu na tayari ajira zaidi ya 80 zimeshatolewa na kituo hicho".
![]() |
Naibu Waziri akikabidhiwa zawadi ya decoda ya TING |

No comments