THIERRY HENRY KOCHA MSAIDIZI TIMU YA TAIFA YA UBELGIJI
Meneja wa timu ya taifa ya Ubelgiji Roberto Martinez amemtangaza nyota wa zamani wa klabu za Arsenal na Barcelona, Thierry, ambaye pia aling'aa sana akichezea timu ya taifa ya mtangaza kuwa mmoja kati ya wasaidizi wake.
Henry mwenye miaka 39 amefurahia uteuzi huo kupitia ukurasa wake wa Twitter na sasa ataenda kufanya kazi pamoja na Graeme Jones ambaye amekua msaidizi wa kocha Roberto Martinez tangu akiwa Swansea,Wigan na hata Everton.
alikuwa mmoja wa wakufunzi wa timu ya vijana Arsenal lakini akajiuzulu Julai baada ya meneja Arsene Wenger kumwambia kwamba hawezi kufanya kazi hiyo akiwa bado anaendelea kuwa mchanganuzi wa soka kwenye runinga.
Kwa sasa Nyota huyo huchambua soka katika kituo cha luninga cha Sky Sports na pia alifanya kazi na BBC Sport wakati wa Euro 2016 akiachana na Arsenal alikokua akifundisha timu ya vijana baada ya kutofautiana na kocha Arsene Wenger aliyemtaka aachane na kazi ya Uchambuzi abaki na timu pekee.
No comments