SIMBA YAFANYA MAMBO YA HATARI TAIFA MASHABIKI WAPAGAWA,AFC LEOPARDS YAPIGWA 4

Wekundu wa Msimbazi Simba wameadhimisha miaka 80 tangu ilipoanzishwa klabu hiyo kwa kuikandamiza AFC Leopards ya Kenya kwa bao 4-0.


Simba ambayo kila tarehe 8 Agosti ya kila mwaka huadhimisha siku maalumu ya klabu hiyo maarufu kama SIMBA DAY na mwaka huu kulikua pia zoezi la kukata keki zoezi ambalo lilisimamiwa na aliyekua Mwenyekiti wa zamani wa klabu hiyo Hasani Dalali.

Katika tamasha la leo lilitawaliwa na matukio mengi ya kupendeza yakiwemo kutambulisha jezi mpya pamoja na wachezaji wapya akiwemo mchezaji Laudit Mavugo ambaye alitawala vichwa vya habari wakati wa usajili wake.

Mchezo wenyewe ulikua mzuri na wa kuvutia huku wachezaji wa Simba wapya wakionekana wataisaidia vilivyo Simba msimu huu huku timu ikicheza kwa kuelewana na kwa kasi kubwa 

Ibrahim Ajib alifunga bao la kuongoza dakika ya 38 goli ambalo lilidumu mpaka mapumziko huku Fredrick Bagnon mshambuliaji toka Ivory Coast akiongoza safu ya ushambuliaji ya Simba.

Kipindi cha pili Simba iliongeza kasi katika kushambulia na kupata mabao mengine matatu bao la pili likifungwa tena na Ajib kisha Shiza Kichuya akafunga bao la tatu huku Laudit Mavugo akifunga bao la 4.

No comments

Powered by Blogger.