LEO NI SIMBA DAY,WEKUNDU WA MSIMBAZI KUTAMBULISHA JEZI MPYA NA WACHEZAJI WAPYA UWANJA WA TAIFA

Kilele cha sherehe za Simba ni leo katika uwanja wa Taifa ambapo wekundu hao wa Msimbazi wataadhimisha tamasha kubwa la Simba Day.


MO alikua mgeni rasmi Simba Day mwaka jana

Simba Day ni hitimisho la wiki nzima ya utaratibu uliowekwa na klabu katika kujitambulisha na kufanya shughuli mbalimbali za kijamii kabla ya msimu mpya kuanza.

Leo katika dimba la Taifa jijini Dar es Salaam licha ya Simba kutambulisha jezi zao mpya na wachezaji wapya lakini pia watacheza mchezo wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya AFC Leopards ya Kenya.

Katika tamasha kama hili mwaka uliopita Simba waliifunga Sports Club Villa ya Uganda kwa bao 1-0 bao pekee la kiungo Awadh Juma dakika za mwisho kipindi cha pili.

Tamasha la mwaka huu limetawaliwa na Mabadiliko ya mfumo ambao Simba wameridhia kuufata katika uendeshaji wa klabu yao.

Mgeni Rasmi anatarajiwa kuwa mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mheshimiwa Paul Makonda

No comments

Powered by Blogger.