"SHAMBA LA BIBI" SASA RUKSA KUTUMIKA, WAZIRI NAPE AKABIDHIWA RASMI LEO
Burudani imerejea Rasmi ndani ya uwanja wa zamani wa Taifa maarufu kama shamba la bibi au uwanja wa Uhuru baada ya serikali leo kupitia kwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye kukabidhiwa rasmi uwanja huo..
Nape alikabidhiwa uwanja huo leo Jumatatu toka kwa kampuni ya Ujenzi toka China ya Beijing Construction Engineering Group Company Limited, (BCEG), na mshauri mwelekezi wa uwanja huo kampuni ya kizalendo chini ya uongozi wa ke, Injinia Aloyce Peter Mushi.
Waziri Nape aliwataka watumiaji wa uwanja huo kulipa ada za matumizi kama inavyostahili, ili hatimaye fedha hizo ziweze kugharimia matunzo ya uwanja huo wenye historia kubwa kwa Taifa letu.
Uwanja huo ambao tangu Mei 22 mwaka jana ulishakamilika hivi sasa una uwezo wa kuchukua mashabiki Elfu 22 na hii ni kutoka katika taarifa ya Injinia Aloyce Peter Mushi.
Naye Meneja Mkuu wa Kampuni ya BCAG, Cheng Long Hai, alisema, uwanja huo umewekewa mifumo yote muhimu kama vile tangi la kuhifadhia maji na mifumo ya maji taka, na kuishukuru serikaliya Tanzania kwa kuiamini kampuni yake kutekeleza mradi huo mkubwa.
Ukarabati mkubwa katika uwanja huo ulihusisha ujenzi wa jukwaa na paa, ikiwa ni pamoja na miundombinu mingine ya uwanja kama vile, mifumo ya kusambaza maji, na kutoa maji taka, uwekaji wa tanki la kuhifadhia maji, pamoja na ujenzi wa vyoo vya kutosha uwanjani.
Baada ya Serikali kukabidhiwa Uwanja wa Uhuru sasa mechi zote za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kuanzia wikiendi hii zinahama Uwanja wa Taifa isipokua mechi kubwa ambazo zitachezwa uwanja wa Taifa mkubwa.

No comments