SERENGETI BOYS KANYAGA TWENDE, YAITUPA NJE AFRIKA KUSINI
Timu ya Taifa ya vijana ya Tanzania chini ya miaka 17 Serengeti Boys leo imeitupa nje Afrika Kusini chini ya umri huo kwa kuwachapa bao 2-0.
Mchezo huo wa kuwania kufuzu kwa fainali za michuano ya kombe la mataifa ya Afrika kwa vijana nchini Madagascar mwakani.
Serengeti Boys sasa imebakiza hatua moja tu ya kuvuka kabla ya kuelekea katika fainali hizo na ili kuvuka hapo itatakiwa kucheza mechi ya mwisho dhidi ya mshindi baina ya Congo Brazaville na Namibia.
Magoli ya Serengeti Boys yalifungwa na Mohamed Rashid Abdallah na Muhsin Malima Makame na kuifanya Serengeti Boys kuing'oa Afrika Kusini kwa jumla ya magoli 3-1 baada ya kutoka sare ya bao 1-1 nchini Afrika Kusini.

No comments