MIRABA SABA YA CHARDBOY77 KWENYE LIGI KUU YA ENGLAND
Na Richard Leonce
Leo Kwenye miraba saba tunatazama mambo mbalimbali ya kitakwimu kwenye michezo ya ligi kuu ya England iliyochezwa jana Agosti 20.
Karibu....
1. Mara ya mwisho kwa mchezo wa Arsenal na Leicester kutoa sare ya 0-0 kabla ya jana ilikua mwaka 2001.
Arsenal hawajawahi kupoteza mchezo wowote wa ligi kuu kwenye uwanja wa King Power. Kwenye mchezo wa jana, Leicester walipiga shuti lao la kwanza lililolenga bao kwenye dakika ya 92 ya mchezo. Mpaka sasa, Jamie Vardy hajapiga shuti lolote langoni tangu ligi ianze.
2. Sergio Aguero amewafunga Stoke City mara 8 katika michezo 7 ya ligi kuu aliyokutana nao.
3. Ushindi wa 2-0 walioupata Burnley jana, ni ushindi wao wa kwanza dhidi ya Liverpool tangu mwaka 1974. Sam Vokes anakua mchezaji wa kwanza kufunga goli dhidi ya Liverpool kwenye uwanja wa Turf Moore tangu Machi 1975.
4. Ushindi wa ugenini wa 0-2 waliopata Hull City dhidi ya Swansea unamaanisha kwamba Hull wanakua timu ya pili iliyopanda daraja kushinda michezo miwili ya ufunguzi, ya kwanza ni Bolton iliyofanya hivyo msimu wa 2001/02.
5. Goli la Victor Wanyama kwenye ushindi wa 1-0 walioupata Tottenham dhidi ya Crystal Palace jana ni la pili kati ya michezo 55 ya ligi kuu ya England aliyocheza mpaka sasa. Crystal Palace wameshinda mara mbili tu katika michezo 21 ya ligi kuu waliyocheza ndani ya mwaka 2016.
6. Katika michezo 32 iliyopita akiwa kocha, Antonio Conte amepoteza mchezo mmoja tu. Ameshinda 29 na kutoa sare mbili. Katika michezo 8 iliyopita ya Chelsea wakiwa ugenini, ni mchezo mmoja tu ndiyo hawakuruhusu nyavu zao kuguswa.
Cesc Fabregas amefikisha assist 26 tangu arejee England, nyingi zaidi ya mchezaji yeyote kwa kipindi hicho. Eden Hazard yeye ametoa assist 1 tu kwenye michezo 26 iliyopita.
7. Kevin Miralas amefunga mabao matatu kwenye michezo mitano iliyopita. Ni sawa na aliyofunga kwenye michezo 25 hapo kabla.
No comments