RASMI : YANGA SASA NI MALI YA MANJI KWA MIAKA 10 IJAYO

Mkutano wa wanachama wa klabu ya Yanga uliofanyika leo jijini Dar es Salaam umeridhia kumkodisha klabu hiyo Mwenyekiti wao,Yusuf Manji kwa miaka 10 kuanzia leo.


Manji ameomba apewe klabu kwa miaka 10 na katika kipindi hicho atakuwa anachukua asilimia 75 ya mapato ya timu, huku asilimia 25 ikibaki kwa wanachama huku akitaka nembo ya klabu na timu kiwa chini yake wakati mambo mengine yatabaki kwa wanachama.

Katika mkutano huo uliofanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee umeshuhudia pia wanachama watatu wa klabu hiyo, Ayoub Nyenzi, Salum Mkemi na Hashim Abdallah wakifukuzwa na kufutiwa uanachama kutokana na utovu wa nidhamu.

Manji aliwaambia wanachama hayuko tayari kufanya kazi na Wajumbe hao wa Kamati yaUtendaji na akaomba wanachama wanaowataka wajitokeze kupiga kura, lakini hakuna aliyeinuka.


No comments

Powered by Blogger.