BARCELONA YAKUMBANA NA KIPIGO KIZITO TOKA KWA LIVERPOOL

Mabingwa wa Spain Barcelona wamekumbana na kipigo kizito cha bao 4-0 toka kwa Liverpool katika pambano lililomalizika hivi punde katika dimba la Wembley.


Mchezo huo wa kujiandaa na msimu mpya wa ligi ulikua wa mwisho kwa timu hizo katika michuano ya International Champions Cup kanda ya Marekani.

Barcelona ambayo ilichezesha nyota wake wote wanaotamba katika kuzifumania nyavu akiwemo mchezaji bora wa dunia Lionel Messi na Luis Suarez walijikuta mpaka kipindi cha kwanza kinamalizika wakiwa tayari washapigwa bao 1-0.

Magoli ya Liverpool yalifungwa na Sadio Mane dakika ya 15, Kisha Mascherano akajifunga bao dakika ya 47 kabla ya Divock Origi hajafunga bao la 3 dakika ya 48 na lile la nne lililofungwa na Marko Grujic dakika ya 90.

Kwa matokeo hayo PSG ambayo ina pointi 9 katika michuano hiyo kanda ya Marekani ndiyo mabingwa wa kanda hiyo.

No comments

Powered by Blogger.