MOURINHO "AMPA" VAN GAAL NGAO YA JAMII, AJITETEA KUMTOA MATA

Kocha wa Manchester United Jose Mourinho amesema ushindi wa ngao ya Jamii ni zawadi kwa Louis Van Gaal aliyekua kocha wa Man United msimu uliopita.


"Tusingecheza hapa kama sio juhudi za Van Gaal kuchukua ubingwa wa FA msimu uliopita na wachezaji pia ambao wachache hawakuwepo kikosini"

Man United iliibuka na ushindi wa bao 2-1 katika mchezo huo dhidi ya mabingwa wa ligi kuu Leicester City magoli ya Jesse Lingard na Zlatan Ibrahimovic huku Jarmie Vardy akifunga bao pekee la City.

Kuhusu Mata kuingia na kutolewa Mourinho amesema "Dakika 4 za mwisho zilikua ni za kulinda goli na Leicester City walikua wakitumia mipira mirefu na ndo mana hakumtIbrahimovic wala Ibrahimovic na kafikiria kumtoa Mata kwakua umbo lake ni dogo na akaingia Mikitaryan ili kuwazuia Leicester City wasicheze mipira mirefu ya juu"

United sasa inajipanga rasmi kwaajili ya mechi ya ufunguzi dhidi ya Bournemouth Jumapili.

No comments

Powered by Blogger.