LICHA YA USHINDI DHIDI YA MAN CITY, ARSENAL YAONGEZA IDADI YA MAJERUHI KIKOSINI

Licha ya ushindi wa bao 3-2 walioupata Arsenal jana wakiifunga Manchester City bado majeruhi yameendelea kukiandama kikosi hicho cha Kocha Arsene Wenger.



Beki wake wa kati Gabriel Paulista aulimia katika dakika za nyongeza za mechi hiyo iliyopigwa nchini Sweden baada ya kugongana na mshambuliaji wa City Kelechi Iheanacho.

Gabriel alitolewa uwanjani kwa machela huku akionekana mwenye maumivu makali hali inayoashiria anaweza akawa nje majuma kadhaa.

Arsenal imepata majeruhi huyu katika safu yake ya ulinzi siku chache baada ya Per Metasacker nae kuumia huku Laurent Koscienly bado haijulikani atarudi lini.

Wenger kaongea baada ya mechi hiyo "Tuliwaomba mara zote katika mechi hizi za kirafiki kutoweka muda wa majeruhi lakini refa aliweka na Gabriel akaumia muda huo"

Kuhusu kununua beki sasa baada ya kuumia kwa Gabriel na hasa kuhusishwa na beki wa Valencia Shkodran Mustafi mwenye thamani ya paundi milioni 40 Wenger anasema,

"Nimeshasema mara nyingi tuko katika soko tunatafuta japokua sio soko rahisi kiasi hicho kwa upande wetu tutegemee habari nzuri hivi karibuni"

Katika mechi ya jana Alex Iwobi,Chuba Akpom na Theo Walcot wote walifunga kwa upande wa Arsenal huku Sergio Aguero na Ikechi Iheanacho wakifunga upande wa City.

No comments

Powered by Blogger.