MESSI NA SUAREZ WAIBEBA BARCELONA KUSHINDA DHIDI YA SAMPDORIA

Mchezaji bora wa dunia Lionel Messi na mshambuliaji Luis Suarez jana waliibeba Barcelona katika ushindi wa bao 3-2 dhidi ya Sampdoria ya Italia.




Luis Suarez alifunga bao la kwanza dakika ya 16 kabla ya Messi hajafunga mabao mawili dakika ya 21 na 34 huku wageni Sampdoria wakipata magoli yao kupitia kwa Luis Muriel na Ante Budimir.

Katika mchezo huo uliopigwa kwenye dimba la Nou Camp jijini Barcelona wenyeji waliweza kuwatambulisha wachezaji wapya Denis Suarez,Samuel Umtiti,Lucas Digne na Andre Gomes.

No comments

Powered by Blogger.