MABINGWA ULAYA : ARSENAL WAKO NA PSG, MAN CITY NA BARCELONA HUKU REAL MADRID WAKIPANGWA NA DORTMUND

Makundi ya ligi ya mabingwa barani yamepangwa jioni ya leo huko Ufaransa na kushuhudia timu zikiangukia katika makundi ambayo yataleta mvuto mkubwa katika hatua hii.


Arsenal wao wako kundi A wakiwa pia na mabingwa wa Ufaransa PSG, FC Basel ya Uswiss na Ludogorets ya Bulgaria kundi ambalo wengi wanazipa nafasi Arsenal na PSG kusonga mbele.

Manchester City wao wamepangwa katika kundi C wakiwa na Mabingwa wa Spain Barcelona,Mabingwa wa Scotland Celtic pamoja na Borussia Mondnglebach ya Ujerumani. Kundi linaloonekana kuwa gumu kutokana na uimara wa timu zenyewe lakini hasa uwepo wa Pep Guadiola katika kikosi cha Man City.

Mabingwa watetezi Real Madrid wamepangwa kukutana na Borussia Dortmund ya Ujerumani, Sporting Lisbon ya Ureno na Legia Warsaw ya Poland.

MAKUNDI YOTE YA MICHUANO HIYO


No comments

Powered by Blogger.