MASHABIKI MAN UNITED WALAUMU POGBA KUTOCHEZA MECHI YA KWANZA JUMAPILI

Mashabiki wa klabu ya Manchester United ya England wamelaumu utaratibu wa kumzuia kiungo wao mpya Paul Pogba kucheza katika mechi ya ufunguzi wa ligi kuu ya England dhidi ya Bournemouth siku ya Jumapili.


Pogba aliyesajiliwa na United wiki hii ataikosa mechi hiyo ya ufunguzi kwa kile kilichoelezwa na chama cha soka cha England FA kwamba alipata kadi mbili za njano katika mechi za mwisho huko Italia katika michuano ya Copa Italia.

Hivyo basi mechi ya kwanza ya Pogba pengine itakua ile mechi ya Ijumaa usiku dhidi ya Southampton katika dimba la Old Trafford.

Mashabiki wengi wa United ambao mtandao huu uliwahoji walichukizwa na hatua ya Pogba kukosa mechi  hiyo kwakua ni ligi tofauti na wakahoji kama wachezaji wote wanaoingia England kama wanaangaliwa kuhusu hilo.

No comments

Powered by Blogger.