KIMEO: ACACIA WATANGAZA KUVUNJA MKATABA NA STAND UNITED

Sakata la utata wa uongozi katika klabu ya Stand United limeingia hatua mbaya zaidi baada ya Kampuni ya uchimbaji madini ya Acacia ya mkoani Shinyanga ambao ni wadhamini wakuu wa klabu ya hiyo maarufu kama Chama la Wana kutangaza kuvunja mkataba wa udhamini.


Katika taarifa iliyotolewa na uongozi wa kampuni hiyo Acacia wameipa Stand United notisi ya miezi mitatu ili kuweza kuvunja mkataba wa miaka miwili ulioingiwa baina ya Stand na Acacia.

Udhamini wa Acacia unaotajwa kufikia bilioni 3 unazungumzwa kama ndiyo sababu ya chokochoko ndani ya klabu hiyo na kupelekea kuibuka kwa makundi mawili lile asilia na kampuni.

Tayari TFF walishasema wawakilishi wa  wanachama wa pande zote mbili wakutane na kutatua mgogoro huo japokua upande wa kampuni wao hawataki kulisikia jambo hili.11

No comments

Powered by Blogger.