LIVERPOOL WAAGA KWA KICHAPO MAREKANI.

Mechi ya mwisho ya Liverpool katika ziara yake nchini Marekani imemalizika kwa kichapo cha bao 2-1 toka kwa AS Roma ya Italia.


Roma ilianza kupata bao dakika ya 29 likifungwa na Edin Dzeko baada ya kazi nzuri ya Kevin Strootman kisha Kinda Oluwaseyi Ojo akaisawazishia Liverpool dakika moja kabla ya mapumziko.

Mshambuliaji Mohamed Salah akamalizia ushindi kwa Roma akifunga bao safi dakika ya 63 akitumia makosa ya kipa wa Liverpool Simon Mignolet.

Liverpool sasa inarejea England tayari kwaajili ya msimu mpya wa ligi ambapo itafungua dimba dhidi ya Arsenal.

No comments

Powered by Blogger.