HAKUNA KULALA SIMBA,YAELEKEA DODOMA KUCHEZA NA POLISI JUMAMOSI

Wekundu wa Msimbazi Simba wameamua kutopumzika na kuelekea Dodoma kwaajili ya maandalizi ya mechi zinazofata katika ligi kuu ya soka Tanzania bara.


Akiongea na waandishi wa habari leo Afisa Habari wa Simba Haji Manara kwa niaba ya uongozi wa klabu hiyo amesema lengo la kwenda Dodoma kwanza ni kuitikia mwaliko wa chama cha soka mkoa wa Dodoma DOREFA pia kuwaonyesha mashabiki wao ambao kwa miaka takribani 10 wamekosa uhondo wa ligi kuu.

Simba inatarajia kuondoka Alhamisi hii na kucheza mchezo wa kirafiki siku ya Jumamosi dhidi ya Polisi Dodoma ambayo iko katika ligi daraja la kwanza.


No comments

Powered by Blogger.