EFL : MAN UNITED,LIVERPOOL ZAPATA MTEREMKO, CHELSEA KUWAVAA LEICESTER CITY

Droo ya Hatua ya 3 ya michuano ya kombe la ligi nchini England zamani Capital one Cup imepangwa jana baada ya kukamilika kwa mechi za hatua ya pili.


Manchester United wataanzia ugenini dhidi ya Timu ya Daraja la chini Northampton Town wakati Mabingwa wa Ligi Kuu England Leicester wao wataikabili Chelsea katika mchezo utakaopigwa katika dimba la King Power nyumbani kwa Leicester City.

Liverpool wao wataanzia ugenini dhidi ya Derby County huku Southampton wakicheza na Crystal Palace, Swansea wao watawakabili Mabingwa Watetezi Manchester City wakati Hull City wakisafiri kwenda kuwavaa Stoke City.

Gillingham, ambao waliwatoa Watford Raundi ya Pili, watasafiri kwenda White Hart Lane kucheza na Tottenham, Nottingham Forest, wanaocheza Daraja la Championship, watakuwa Wenyeji wa wa washika mitutu Arsenal.

RATIBA KAMILI


  • Nottingham Forest vs Arsenal
  • Leeds United vs Blackburn Rovers
  • Queens Park Rangers vs Sunderland
  • West Ham vs Accrington Stanley
  • Southampton vs Crystal Palace
  • Swansea vs Manchester City
  • Fulham vs Bristol City
  • Bournemouth vs Preston North End
  • Tottenham vs Gillingham
  • Everton vs Norwich City
  • Derby County vs Liverpool
  • Northampton vs Manchester United
  • Brighton vs Reading
  • Newcastle United vs Wolverhampton Wanderers
  • Stoke City vs Hull City
  • Leicester City vs Chelsea

● Mechi hizi zitachezwa kwenye Wiki ya kuanzia Septemba 19


No comments

Powered by Blogger.