BEKI MPYA ARSENAL AANZA KWA KUFUNGA (+Video highlights za mchezo)

Beki mpya wa Arsenal Rob Holding amefunga bao moja katika ushindi wa bao 3-1 walioupata Arsenal mapema alfajiri ya leo wakiifunga klabu ya Chivas ya Mexico.


Mechi hiyo ya maandalizi ya msimu mpya ilipigwa jijini Los Angeles nchini Marekani ambako Arsenal wameweka kambi kujiandaa na msimu mpya.

Holding aliyeanza katika mchezo huo akicheza pamoja na Colum Chambers kama mabeki wa kati alifunga bao la kwanza dakika ya 34 ya mchezo huku magoli mengine yakifungwa na Alex Oxlaide-Chamberlain na Chuba Akpom.

Video



1 comment:

Powered by Blogger.