WANAOMTAKA NEYMAR KUILIPA BARCELONA PAUNDI MILIONI 210

Mabingwa wa Spain Barcelona wameweka kipengele cha kulipwa kiasi cha paundi milioni 210 kama kuna klabu itataka kumnunua  mshambuliaji wake raia wa Brazil Neymar.

 Barcelona wamemsainisha Neymar Mkataba mpya wa kuendelea kukipiga katika klabu hiyo ya Catalunya  ambao utambakisha klabuni hapo hadi Juni 2021

Kipengele cha kununuliwa kwa kiasi hicho cha pesa ambacho kitavunja rekodi zote za usajili kuwahi kutokea duniani na kuzuia kwa kiwango kikubwa timu kama Manchester United,PSG na Real Madrid ambazo zilikua zikimwania nyota huyo.


Neymar, ambae alibakisha Miaka Miwili kwenye Mkataba wake uliopita sasa atabaki Nou camp mpaka mwaka 2021.

Mkataba huu mpya umewekwa vipengele vyenye kumfunga vilivyo Neymar ikiwa ni pamoja na Barcelona kulipwa Pauni Milioni 167 ikiwa atatakiwa na Klabu nyingine ndani ya Mwaka Mmoja na Dau hilo kupanda hadi Pauni Milioni 185 kwa Mwaka wa Pili  na kufikia Pauni Milioni 210 kwa Miaka Mitatu iliyobaki ya Mkataba huo mpya.

Neymar alimaliza msimu uliopita akiifungia Barcelona magoli 31 katika Mechi 49 na kuisadia Barca kutwaa Ubingwa wa La Liga na Copa del Rey akiwa ameshaichezea Barcelona mechi 141 na kufunga mabao 85 tangu alipojiunga nayo akitokea Santos ya Brazil.




No comments

Powered by Blogger.