VITU NILIVYOVIONA KWENYE MECHI TATU ALIZOCHEZA YANGA.

Mabingwa wa Tanzania bara Yanga wanaendelea na mechi zao za kombe la shirikisho barani Afrika hatua ya Makundi. Kwa upande wangu vitu hivi ndivyo nilivyoviona mpaka sasa.


1: Kuna huu ukweli ambao unaonekana kama siyo ukweli, Tangia Msuva achoke kuibeba Yanga na kuitua kutoka kwenye mabega yake ameshindwa tena kuibeba, Yanga imekuwa nzito kwake tena. Kwanini nasema hivo?
Yanga kwenye hatua hii ilipofikia inahitaji Mshambuliaji wa pembeni ambaye atakuwa anatoa vitu vifuatavyo: Mosi, Awe na uwezo mkubwa wa kufunga wakati wowote, na kusaidizana vizuri na washambuliaji wa kati.

Pili, awe na uwezo wa kutoa pasi za mwisho za Magoli na Krosi zenye madhara. Tatu, Awe ni sehemu sahihi au upande sahihi wa timu kupeleka mipira, ukiangalia mechi ya mwisho , Yanga walikosa sehemu sahihi ya kuwekeza mipira yao. Kwani walipokuwa wanajaribu kupitisha mipira katikati walikuwa wanakutana na lundo la wachezaji wa timu pinzani hali iliyokuwa inawafanya kukosa njia za kupitishia mipira. Ila kama Msuva angekuwa hai ilikuwa ni suala la kuwekeza mipira kwake.

KIPI KIFANYIKE KUTATUA TATIZO HILI ?

Na jua kwenye kila anguko kuna swali ambalo unatakiwa ujiulize siku zote. Kipi umejifunza kwenye kila anguko??? . Kwangu mimi kwenye kila anguko huwa najifunza kuongeza na kuimarisha nidhamu yangu. Ndicho kitu pekee ambacho Msuva anatakiwa afanye. Ni muda mwafaka wa yeye kuimarisha nidhamu yake ya kiuchezaji , siamini kama hawezi tena pata nguvu ya kuibeba Yanga , na kitu kizuri kwake ni kwamba kulia kwake anabeki mzuri ambaye wanauwezo mkubwa wa kusaidizana kwenye majukumu ya kushambulia.

Pili, Juma mahadhi anaweza kuwa mtu mbadala wa kuibeba Yanga kwa upande huu ila atakuwa anakosa kitu kimoja tu nacho uwezo mkubwa wa kufunga. Uliangalia mechi dhidi ya TP Mazembe? Uliona ushirikiano waliokuwa nao na Juma Abdul? Uliona uwezo wake wa kusukuma mashambulizi kwa nguvu, uliona jinsi ambavyo hakuwa anapoteza mipira? Vitu hivyo havikionekana Kwa Msuva kwenye mechi iliyofuata.

2: Siku zote Presha huja pale unapokosa cha kufanya, na ndicho kitu ambacho Yanga wamekuwa wakikumbana nacho. Mfano mzuri ni mechi mbili za mwisho alizocheza nyumbani. Mechi dhidi ya TP Mazambe ule umati ulioingizwa bure uwanjani uliwafanya kuwa na presha kitu ambacho kiliwanyima kitu sahihi cha kufanya kufanya. Waliishia kuwaburudisha mashabiki kwa kupaka rangi mpira. Mpaka pale TP Mazembe walipowakumbusha mchezo wa mpira huamuliwa kwa magoli. Vivyo hivyo kwenye mechi Ya mwisho dhidi ya Medeama.

Baada ya Yanga kushawazishiwa Goli, kitu kilichoingia kwenye akili yao ni Presha. Tena Presha ilizidi zaidi pale walipokosa njia za kupitishia mipira kuelekea kufunga, ndiyo maana kuna wakati walikuwa wakipata nafasi za kufunga na kuwa na kitete kwa kutokuamini kuwa wamepata nafasi kama hizo , mwisho wa siku wakawa wanakoswa nafasi za wasi.

KIPI KIFANYIKE KUTATUA TATIZO HILI…???

Najua kocha ndiye mtu pekee anayejua maendeleo ya wachezaji vizuri. Ila kuna kimoja ambacho kinakosekana sana kwenye mechi za Yanga kwa hivi sasa. Uwepo wa kiongozi kama Nadir ndicho kitu cha muhimu kinachokosekana sana. Ni mtu pekee ambaye amekuwa akiwashusha presha wenzake na kuwapa motisha kubwa pindi timu inapopitia kipindi kigumu uwanjani.

3: Kuna vitu vitatu kwenye mpira; Kipaji, Motisha na Mtazamo. Kipaji huonesha ni kipi unaweza kufanya. Motisha huonesha ni kwa njinsi gani una hali nguvu ya kukitumikia kipaji chako, kitu kizuri kuhusu motisha ni kwamba ili uweze kufanya motisha yako iwe juu unatakiwa uondoe vitu vyote visivyokupa motisha. Mtazamo huonesha ni jinsi gani utafanya vizuri. Yanga wana vitu viwili tu navyo ni kipaji na motisha ila wamekosa Mtazamo. Mtazamo wa jinsi gan gani wafanye vizuri, kufanya vizuri hakuishii kuwaweka wachezaji kamba nzuri nchi za nje, kuna mipango zaidi ya hiyo ambayo huonesha utayari wako wa kufanya vizuri.

KIPI KIFANYIKE KWENYE HILI……?????

Wakati mwingine mpira si maisha pekee huenda zaidi ya hapo na ndiyo maana kwenye mpira adui mkubwa wa “BORA” ni jirani yake “NZURI” Kama kila siku utakaa kufanya kufanya kizuri hakika hutokuja kufanya kitu bora. Ni wakati wa Yanga kufanya kitu bora. Ni wakati wa Yanga kuzijua vizuri timu pinzani, Ni wakati wa Yanga kucheza kwa malengo , wameshindwa kujua jinsi ya kucheza nyumbani, wamecheza vizuri nyumbani wanatakiwa wawe bora ugenini kwa mechi zilizobaki.

4: Tatizo jingine ambalo ni kubwa ni kukosa kiungo halisi wa eneo la ukabaji. Viungo wanaoanza kwenye mechi za Yanga eneo hilo siyo la kwao. Kitu hiki kilikuwa chanzo kikubwa kwa Yanga kukosa ushindi dhidi ya TP Mazembe. Kamusoko alicheza nyuma sana, hali iliyosababisha asiwe na uwezo wa kuwalisha washambuliaji, mechi iliyofuata Mbuyu alichezeshwa eneo lile na kumpa uhuru Kamusoko kufanya alichopewa na Mungu mpaka akatoa pasi ya mwisho kwa Ngoma. Kitu ambacho kilikosekana kwa Mbuyu ni kwamba , hakuwa na uwezo mkubwa wa kupiga pasi nyingi yani kusambaza mipira kwenye timu, pili Pindi Yanga ilipokuwa inashambuliwa kwa kasi , Mbuyu alikuwa anazidiwa kasi hali iliyokuwa inamlazimu kufanya madhambi kitu ambacho ni hatari kwani anaweza pewa kadi itakayomgharimu timu. Tatu , Mbuyu akiwa anacheza eneo la kati la ukabaji, mwili huonekana eneo lile lakini akili na uchezaji wake huwa kama beki wa kati.

5:Pia tatizo jingine lipo upande wa beki ya kushoto , kitu ambacho nimekosa jibu tangia nianze kumuona Oscar Joshua ni kwanini yuko pale Yanga? Ni kwanini huwa anaitwa timu ya Taifa? Uchezaji wake ni wa mchangani, mipira mingi hubutua sana, ni mwepesi kuishiwa pumzi, hana kasi, si mzuri anaposhambulia. Ni wazi Mwinyi Haji ni mhimili mkubwa wa eneo hili.

Nimekuwa nikiishi kwa kuamini kuwa kupanda( growing) na na kukua (Growing up ) lakini Yanga wamenionesha utofauti wa neno Growing na Growing Up.

Ahsanteni , Mungu awabariki.

Martin Kiyumbi ( 0657 77 10 77, 0744 08 08 91).

No comments

Powered by Blogger.