TATHMINI KUELEKEA MCHEZO WA YANGA NA MEDEAMA LEO

Na Ayoub Hinjo

Ni mchezo mmoja kati ya minne ambayo timu ya Yanga amebakiwa nayo,ni hivyo hivyo kwa Medeama kutoka nchini Ghana. Kwa kuzitazama timu zote mbili unaweza kugundua ndio timu pekee zilizofungwa katika kundi lao lenye TP Mazembe ya Congo na Mo Bejaia ya Algeria.

Kuelekea mchezo huo muhimu kwa Yanga. Mchezo ambao ni wa lazima kupata matokeo chanya tena kwa idadi kubwa ya magoli kama itawezekana hili kuweka wigo mpana pale litakapokuja jambo la kufuzu kwa tofauti ya magoli.

Dhidi ya TP Mazembe ulikuwa huwezi kuona ubora wa Kamusoko ambaye alikuwa anacheza chini zaidi kwa kuwalinda mabeki wanne. Ilikuwa ni kamari ambayo haikufanikiwa kuipa Yanga matokeo sababu ubora wa Kamusoko unaonekana mara nyingi timu inapokuwa inafanya mashambulizi. Ubora wa Kamusoko upo katika kuchezesha timu na kutengeneza nafasi kwa washambuliaji.

Ni vyema kama kiungo mkabaji wa asili kama Twite,Makapu au Ngonyani mmoja wao akapewa nafasi na kisha kumsogeza Kamusoko juu ambako atakuwa huru kusambaza mipira. Uwepo wa Msuva utakuwa na nyongeza kwa Yanga ambao walikosa huduma yake kwenye mechi iliyopita. Msuva ana uwezo wa kukimbia nyuma ya mabeki na kufanya maamuzi.

Hatujawahi kuwaona Medeama wakicheza lakini ni vyema kuwa na uangalifu zaidi na washambuliaji wao sababu tumeshuhudia Yanga wakipoteza michezo miwili kwa mabeki kukosa umakini ndio maana wanasema "unapomkimbiza mwizi hakikisha unafunga mlango".

Kiuhalisia mechi haitokuwa ya upande mmoja sababu Medeama anahitaji matokeo ili afufue uwezekano wa kufuzu pia ni hivyo hivyo kwa Yanga ambao wamepoteza michezo miwili ya awali.

No comments

Powered by Blogger.