SHERIA ZA SPAIN ZAWANUSURU MESSI NA BABA YAKE KUFUNGWA GEREZANI
Hukumu hiyo imetolewa muda mchache uliopita ila imekua faida kwao kwani wawili hao hawataenda gerezani kama hukumu hiyo inavyoelekeza kwani Sheria za Spain haziruhusu mtu aliyefungwa chini ya miaka miwili kutumikia kifungo chake gerezani pia wawili hao hawana rekodi yakuwa na makosa.
Kwahiyo badala ya kwenda gerezani wametakiwa kulipa faini kila mmoja Messi akitakiwa kulipa paundi milioni 1.7 wakati baba yake atatakiwa kulipa faini ya paundi milioni 1.3.
Messi na baba yake walikutwa na hatia ya kukosa kulipa kodi inayokadiriwa kufikia paundi milioni 3.2 na paundi milioni 4.6 kati ya mwaka 2007 mpaka 2009.
No comments