JOHN STONES "AJIPELEKA" MANCHESTER CITY
Mlinzi wa kati wa klabu ya Everton John Stones ameiambia klabu yake hiyo kwamba anataka kujiunga na Manchester City katika dirisha hili la usajili.
Everton wanataka paundi milioni 50 kwa timu yoyote inayomtaka mchezaji huyo kiasi ambacho kitamfanya kuwa beki ghali zaidi katika historia ya soka la England.
Stones ni mmoja kati ya mabeki wanaowindwa vilivyo na kocha mpya wa Manchester City Pep Guadiola katika ujenzi mpya wa klabu hiyo.
Joitafikiwa mwenye miaka 22 anajaribu kulazimisha uhamisho huo ufanikiwe huku Everton wakisema watamruhusu tu iwapo bei hiyo itafikiwa.
Stones alikua mmoja kati ya walinzi wa kati walioitwa na kocha Roy Hodgson katika kikosi cha England kwenye mashindano ya Euro 2016 nchini Ufaransa lakini hakucheza mechi yoyote.
Alijiunga na Everton January 2013 akitokea Barnsley kwa ada ya uhamisho wa paundi milioni 3 tu.

No comments