SAMATTA APIGA BAO 1 GENK IKISHINDA NYUMBANI KATIKA MICHUANO YA EUROPA LEAGUE
Mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania na nahodha wa Taifa Stars Mbwana Samatta jana usiku aliweka historia mpya katika maisha yake ya soka.
Akiwa ndiye Mtanzania wa kwanza kucheza katika michuano ya Europa League Samatta aliweza kufunga bao 1 kati ya mabao mawili ya timu yake ya Genk ilipoifunga Buducnost ya Montenegro.
Mchezo huo wa raundi ya pili ya michuano hiyo ya pili kwa ukubwa katika ngazi ya klabu barani Ulaya baada ya ile ya Ligi ya mabingws Ulaya ulichezwa nyumbani kwa Genk.
Genk walipata bao la kwanza kwa njia ya penati iliyofungwa na kiungo raia wa Congo DRC Neeskens Kebano dakika ya 17 wakati Mbwana yeye alifunga dakika ya 79.
Mchezo wa marudiano utapigwa Alhamis ijayo huko Montenegro ambapo Genk watatakiwa kulinda ushindi wao ili kutinga hatua ya tatu.
Samatta akipongezwa na wachezaji wenzake |

No comments