MASIKINI DR. TIBOROHA : TFF YAIPIGA "STOP" STAND UNITED KAMPUNI ANAYOIONGOZA

Shirikisho la soka Nchini Tanzania TFF limesimamisha uongozi wa klabu ya Stand United Kampuni chini ya Mtendaji wake mkuu Aliyekua katibu mkuu wa zamani wa Yanga Dr. Jonas Tiboroha.


 Katika kikao chake cha 13 Julai 2016, Kamati ya Uchaguzi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), imetoa msimamo kuhusu suala la Stand United kama ifuatavyo:-
Kamati imepitia vielelezo vyote na kujadiliana na wadau wa Stand United na kubaini bayana kwamba Stand United Football Club, ndiyo jina sahihi na halali lililosajiliwa kwa Msajili wa Klabu na Vyama vya Michezo.
Uchaguzi uliofanyika hivi karibuni kwenye Klabu ya Stand United una sifa zote za kuitwa uchaguzi huru na wa haki kwa vile mchakato ulihusisha wanachama halali klabu hiyo.
Wanachama wa Stand United ambao hawakushiriki uchaguzi ikiwa ni pamoja na wale waliokwenda kundi la kampuni wana uhalali wa kuendelea kuwa wanachama wa Stand United.
Viongozi waliochaguliwa katika uchaguzi wa Stand United FC ni halali na ni ruksa kwao kuendesha ofisi na shughuli za Stand United kwa ujumla.
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania linatambua daftari la Wanachama wa Stand United lililoboreshwa kwa maelekezo ya TFF.

No comments

Powered by Blogger.