PEP GUADIOLA AANZA NA KICHAPO MAN CITY, CHELSEA NA LIVERPOOL ZASHINDA

Kocha mpya wa Manchester City Pep Guadiola ameanza kibarua chake ndani ya klabu hiyo kwa kichapo cha bao 1-0 dhidi ya Bayern Munich.



Mchezo huo wa kirafiki uliopigwa katika dimba la Allianz Arena jijini Munich Ujerumani ulishuhudia Pep akianzisha kikosi kilichosheheni vijana badae akabadili na kuingiza wakongwe wachache.

Bayern Munich chini ya kocha mpya Carlo Ancellot ilionekana kutawala mchezo huo lakini Umahiri wa kipa wa City Willy Cabbalero ulikua kikwazo kupata goli lolote kipindi cha kwanza.

Goli pekee katika mchezo huo lilifungwa na chipukizi Erdal Ozturk dakika ya 76.

Katika mechi nyingine hiyo jana Chelsea wsliibuka na ushindi wa bao 3-0 wakiifunga Wolfsberger AC huku Liverpool wakiifunga Huddersfied bao 2-0.

No comments

Powered by Blogger.