NAMBA ZA WACHEZAJI MAN UNITED : MARTIAL AMWACHIA IBRAHIMOVIC LINGARD AMRITHI CHICHARITO, NAMBA 6 YAMSUBIRI POGBA?

Kuelekea msimu mpya wa Ligi kuu nchini England na michezo mbali mbali ya klabu hiyo,namba za jezi za wachezaji zimewekwa wazi.



Antony Martial mmoja kati ya wachezaji waliofanya vizuri msimu uliopita akiibuka kuwa mfungaji bora wa klabu ameachia jezi namba 9 aliyokua akiivaa na sasa jezi hiyo itavaliwa na Zlatan Ibrahimovic aliyesajiliwa kama mchezaji huru.

Martial sasa atavaa jezi namba 11 ambayo amekua akivaa akiwa na timu yake ya Taifa ya Ufaransa huku Adnan Januzaj aliyekua akivaa jezi hiyo akipewa Jezi ya mkongwe Nemanja Vidic namba 15 ambayo ilikua haivaliwi na mtu.

Marcus Rashford yeye amepewa jezi namba 19 iliyokua ikivaliwa na James Wilson huku Jesse Lingard akikabidhiwa jezi iliyokua ikivaliwa na Javier Hernandez Chicharito.

Mchezaji mpya anayecheza kama beki wa kati Eric Bailly amekabidhiwa jezi namba 3 huku Henrik MiMikityar akipewa namba 22.

Katika hali nyingine namba 6 imeonekana haina mtu huku Wapenda Soka wakitabiri kwamba inasubiri uhamisho wa Paul Pogba ambaye mpaka sasa hakijaeleweka.



No comments

Powered by Blogger.