ICC: MAN UNITED YABUGIZWA BAO 4-1 NA BORRUSIA DORTMUND

Ziara ya Manchester United nchini China imeanza vibaya baada ya kukumbana na kipigo cha bao 4-1 toka kwa Borussia Dortmund ya Ujerumani.


Mchezo huo wa kirafiki lakini pia wa kuwania kombe la ICC ulipigwa jijini Shanghai China.

Mpaka mapumziko tayari United ilishafungwa bao 2-0 Magoli ya Gonzalo Castro na lile la penati ya Pierre-Emenike Aubemeyang.

Kipindi cha pili Dortmund waliongeza bao la 3 likifungwa na Dembele kabla ya Henrik Mikytaryan hajafunga bao la kufutia machozi kwa United na baadae Castro akafunga bao la 4.

No comments

Powered by Blogger.