HEh! KUMBE REAL MADRID NAO BADO WANAMWANIA POGBA

Sakata la usajili wa kiungo Mfaransa Paul Pogba limeingia katika hatua nyingine baada ya Real Madrid kushindwa kukataa kama hawamuhitaji mchezaji huyo.



Kocha wa Real Madrid  Zinedine Zidane amekataa kuthibitisha kwamba wana mpango wa kumsajili Pogba.

Man United ndiyo timu inayotajwa mno kumwania Pogba huku wakipandisha dau lao toka paundi milioni 86 mpaka paundi milioni 92 wakitarajia kumlipa paundi 200,000 kwa wiki.

Pogba ambaye inasemekana anaihusudu vilivyo Real Madrid yawezekana tukasikia ametimkia Real Madrid na hii pengine itachangiwa na uwepo wa Zidane katika kikosi cha Madrid japokua taarifa zingine zinadai kwamba Man United wameshamalizana na Pogba.

No comments

Powered by Blogger.