CELTIC YAMSAJILI KOLO TOURE TOKA LIVERPOOL

Mabingwa wa Scotland Klabu ya Celtic imekamilisha usajili wa beki wa kimataifa wa Ivory Coast Kolo Toure toka Liverpool.



Toure mwenye miaka 35  ambaye ni kaka wa kiungo wa Manchester City Yaya Toure amesaini mkataba wa mwaka mmoja kuichezea Celtic inayoshiriki ligi ya mabingwa barani Ulaya ikianzia katika hatua ya pili ya mtoano.

Usajili wa Toure unamuunganisha na kocha wake wa zamani Brendan Rodgers ambaye alimsajili akiwa Liverpool alipoachwa na Manchester City.


No comments

Powered by Blogger.