BAADA YA KITEMWA YANGA, SALUM TELELA ASAINI KUICHEZEA NDANDA FC YA MTWARA

Aliyekua kiungo wa mabingwa wa Tanzania bara Yanga na timu ya Taifa ya Tanzania Salum Telela amesaini kuichezea Ndanda FC ya Mtwara.


Telela aliyeachwa na Yanga katika dirisha hili la Usajili linaloendelea amesaini kuichezea Ndanda FC inayotumiwa uwanja wa Nangwanda Mtwara kwa mkataba wa mwaka mmoja.

Awali Telela ilisemekana ameamua kurudi shule baada ya kuachwa na Yanga lakini maamuzi hayo sasa yamegeuka ndani ya siku hizi chache na rasmi ameamua kujiunga na Ndanda FC.

No comments

Powered by Blogger.