ALICHOSEMA MOURINHO BAADA YA MECHI YA MAN UNITED NA MAN CITY KUFUTWA

Pambano la watani wa jadi wa jiji la Manchester Yani klabu mbili za Manchester United na Manchester City limefutwa kutokana na hali mbaya ya hewa iliyoathiri uwanja wa "kiota cha ndege" jijini Beijing China.


Mechi hiyo ya aina yake ilikua ya kwanza katika historia ya timu hizo kufanyika nje ya England lakini sasa majaliwa ya kuona historia mpya ikiwekwa imefutika baada ya uwanja kutokua na hali nzuri ya kuruhusu mechi hiyo kufanyika.

Kocha wa Manchester United amenukuliwa akisema kwamba "Hali ya uwanja na hali ya wachezaji wangu ndiyo mambo ya msingi ninayoyatazama katika mechi za maandalizi kuliko matokeo ya mechi zenyewe hivyo basi kama utaniuliza nini tufanye nitasema tuwarudishe wachezaji nyumbani wakiwa hawana majeraha"

Zaidi ya wafanyakazi 70 wa uwanja huo wamekua wakihangaika kuweza kutatua changamoto mbalimbali za uwanja ili mechi iweze kufanyika bila mafanikio.

Manchester City wao watasafiri kwenda katika mji wa Guangdong China kwaajili ya mechi yao ya Alhamisi dhidi ya Borussia Dortmund wakati United watarudi jijini Manchester.

Timu zote hizi zitakua kambini Gothenburg nchini Sweden ambapo United itacheza na Galatasaray Julai 30 wakati Man City wao watacheza na Arsenal Agosti 7.

No comments

Powered by Blogger.