AZAM FC YALETA MSHAMBULIAJI MWINGINE TOKA IVORY COAST..

Maandalizi ya msimu mpya wa  ligi kuu nchini Tanzania yanaendelea vyema kwa kila klabu kutaka kujiweka sawa kuonyesha makali yake msimu ujao.




 Wana lambalamba Azam FC wao wamemleta nchini Mshambuliaji Raia wa Ivory Coast Ibrahima Fofana kwaajili ya majaribio ya kuichezea klabu hiyo yenye maskani yake Chamazi jijini Dar es Salaam.

Fofana mwenye miaka 26 ametua nchini mchana wa leo akitokea akitokea timu ya Union Sportive ya Tunisia ambako alijiunga baada ya kutoka klabu ya Asec Memosas ya Ivory Coast.

Kama mshambuliaji huyo atafanikiwa katika majaribio yake anaweza kusaini mkataba wa miaka miwili kuwatumikia wawakilishi hao wa Tanzania katika michuano ya kombe la Shirikisho barani Afrika mwakani.

Tayari Azam FC wana wachezaji wawili toka Ivory Coast ambao ni ndugu Kipre Tchetche na Kipre Balou.


No comments

Powered by Blogger.