YANGA YAANZA ROBO FAINALI KOMBE LA SHIRIKISHO KWA KUFUNGWA NA WAARABU
Mabingwa wa Tanzania bara na wawakilishi wa nchi katika kombe la shirikisho barani Afrika Yanga wameanza vibaya mechi za kundi A katika kombe la shirikisho.
Mabingwa hao wa Tanzania bara walio katika kundi A wamepoteza mechi hiyo muhimu kwa kukubali kufungwa bao 1-0 toka kwa wenyeji Mo Bejaia ya Algeria bao pekee la mshambuliaji Sahli.
Ushindi huo unaiweka Timu hiyo ya Algeria katika nafasi ya pili nyuma ya TP Mazembe ambao wao waliifunga Medeama ya Ghana kwa bao 3-1 katika mechi nyingine ya kundi hilo.
Mechi inayofata kwa Yanga itakua nyumbani uwanja wa Taifa kuwakaribisha mabingwa wa Afrika TP Mazembe ya Congo DR huku Mo Bejaia wakisafiri kuwakabili Medeama ya Ghana.

No comments